Friday, 4 November 2011

MHESHIMIWA MNYIKA UNAIFAHAMU BARABARA HII JIMBONI KWAKO?



Mnyika
 Takriban mwaka mzima sasa barabara hii  ya Tandale Uzuri imejaa mashimo na inaonekana kama imesahaulika. Wananchi na watumiaji wa barabara hii nikiwemo mimi najiuliza hivi watendaji wako wapi?

Kwa bahati mbaya au nzuri, barabara hii ipo kwenye Jimbo la Ubungo, Jimbo la John Mnyika ambaye anatokea chama cha Upinzani-CHADEMA, hili ni doa kwa uongozi wake ambao ndio kwanza una mwaka mmoja. Je Mheshimiwa anafahamu kwamba hii barabara ipo hivi? 

"Hali hii inasababisha tukose imani na wanasiasa, kwa kuwa ni mwaka jana tu walikuwa wanazunguka nyumba kwa nyumba wakisaka kura na moja ya ahadi zao ilikuwa kwamba wataboresha barabara, lakini kama uboreshaji wenyewe ndio huu basi naona hakuna haja ya kupiga kura," anasema mpiga kura mmoja wa Sinza ambaye barabara hii ni kero kwake.


Mzee huyu mwenye nguo nyeusi amejitolea kujaza kifusi kwenye barabara na anawatoza madereva kati ya shilingi mia na miambili, kwa sababu watumiaji wanakerwa na hali hii, basi hawana namna lazima watoe, lakini sasa huyu mzee naye hataki kumaliza haraka kwa kuwa hiki sasa kimekua kitega uchumi. (KUFA KUFAANA)


Hapa ukija kichwakichwa unavunja sample.

Kila mtu anapita pembeni, labda kazi ya kujaza kifusi ikikamilika italeta ahueni.

1 comment:

Anonymous said...

Barabara hii inaunganisha jimbo la Ubungo na Kinondoni. Eneo ambalo umepiga picha lipo kwa sehemu kubwa upande wa Jimbo la Kinondoni. Hata hivyo, nilishaitaarifu Manispaa na TANROADS ubovu wa hiyo barabara. Nitaendelea kufuatilia. Mnyika