Tuesday, 1 November 2011

GAMA ALIA NA NJIA ZA PANYA

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro  Mheshimiwa Leonida Gama akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu hali ya upatikanaji wa sukari mkoni Kilimanjaro jana. (Picha na Habari kwa hisani ya mdau, Shabani wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa)




Licha ya juhudi za uongozi wa Mkoa wa Kilimanjaro za kuzuia kupitisha sukari za magendo kwenye mipaka ya mkoa huo na Kenya, usafirishaji umeendelea kwa njia za panya.

Wasafirishaji wa sukari na bidhaa za nafaka kwa njia ya magendo kwa kupitia mipaka ya Holili na Tarakea wilayani Rombo wamebuni njia hizo baada ya kuona ulinzi umeimarishwa mpakani.

Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake jana Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama amesema wafanya biashara hao wameshaanza kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa jambo lilowapekea kubadilisha njia na kujaribu kusafirisha bidhaa hizo kwa kupitia eneo la Ngarenairobi wilayani Siha.

MAGENDO YA MAHINDI

Mpaka kufikia siku ya Ijumaa tayari malori  nane yenye gunia zipatazo 100 za mahindi  kila moja yanashikiliwa na polisi Wilayani Siha  kwa tuhuma za kujaribu kusafirisha nafaka hiyo kwenda nchi jirani kinyume na sheria.

Mwishoni mwa mwezi wa tisa Gama aliendesha zoezi la kudhibiti uvushwaji wa nafaka na sukari katika njia zilizo katika mpaka wa Tarakea na Holili wilayani Rombo.

No comments: