TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea barua ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) yakuomba viongozi wa chama hicho kukutana na Mheshimiwa Rais kuzungumzia Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011.
Mheshimiwa Rais Kikwete amelipokea ombi hilo kwa furaha kwa sababu nijambo jema.
Kufuatia kukubali kwake ombi hilo, Mheshimiwa Rais ameagiza mawasiliano yafanyike ilikupanga tarehe mwafaka ya kukutana na viongozi hao wa CHADEMA na kuzungumzia suala hilo.
IMETOLEWA NA: KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU NOVEMBA 22, 2011 DODOMA |
No comments:
Post a Comment