Hali ya Bwawa la Nyumba ya Mungu, Wilaya ya Mwanga, Kilimanjaro sio nzuri kutokana na kukauka kwa kiasi kikubwa cha maji katika bwawa hilo ikiwa ni matokeo ya mabadiliko ya tabia nchi na uharibifu wa mazingira ulifanywa na shughuli za binadamu.
Akitoa taarifa ya hali ya Bwawa hilo kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mheshimiwa Leonidas Gama Ofisa Mkuu wa Ofisi ya Maji ya Bonde la Mto Pangani Bwana Hamza Sadiki amesema kiwango cha upungufu wa maji katika bwawa hilo kimefikia asilimia 70.
Kwa mujibu wa Bwana Sadiki kina cha maji katika Bwawa hilo kilikuwa mita 683.13 juu ya usawa wa bahari sawa na mita za ujazo milioni 233.27.
Mheshimiwa Gama ameadhimia kufanya ziara juma lijalo katika maeneo ambayo ni vyanzo vya maji vya bwawa hilo ili kujionea hali ya uharibifu wa mazingira katika vyanzo hivyo.
Mkuu wa Mkoa wa KILIManjaro Mheshimiwa Leonidas Gama akiongea na wananchi wanaishi karibu na bwawa la Nyumba ya Mungu wilayani Mwanga |
Sehemu ya Miundombinu ya kuzalishia umeme katika bwawa la Nyumba ya Mungu |
No comments:
Post a Comment