Karafuu |
Wakulima wa zao la Karafuu Zanzibar wametakiwa kutokuwa na wasiwasi wa kununuliwa Karafuu zao kwani Serikali ina fedha za kutosha za kununulia zao hilo.
Akizungumza katika Baraza la Idd ALhaj lililofanyika leo (jana) huko katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete Pemba Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk Ali Mohamed Shein amesema kuwa wananchi wasidanganyike na uzushi ulioenezwa baadhi ya watu kuwa Serikali haina fedha zakutosha za kununulia karafuu jambao ambao sio kweli ni la uzushi na uongo mtupu.
Amesema kuwa Serikali imefarajika kwa jitihada za Wakulima kwa kuuza karafuu zao katika vituo vya Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar(ZSTC) ambapo hadi juzi jumla ya tani 2136.91 zenye thamani ya shilingi zaidi ya Billioni 31 zimeshanunuliwa kutoka kwa Wakulima.
Alhaj Shein ametowa wito kwa Wakulima kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali kuacha kuuza karafuu
kwani kufawa njia ya Magendo kwani kufanya hivyo tutakuwa tumeuhami uchumi wetu ambao ni tegemeo kwa Taifa zima.
Aidha Dk Shein amevitaka Vyombo vya Ulinzi kuongeza jitihada zake za kupambana na Magendo ya Karafuu.
Akizungumzia juu ya usafirishaji wa Mahujaji wa Zanzibar wanaokwenda Mecca kuhiji Alhaj Shein amewataka mawakala wa Mashirika yanayosafirisha Mahujaji kwaajili yakutekeleza ibada ya Hijja kuondowa usumbufu kwa Mahujaji hao.
Amesema pamoja na kuwa idadi ya Mahujaji wa Zanzibar inaongezeka kila mwaka lakini kuna baadhi ya Mahujaji hupata usumbufu katika kutekeleza ibada hiyo kutoka kwa baadhi ya Taasisi zinazosafirisha Mahujaji.
Vile vile amezitaka Taasisi zinazoshughulikia safari za Hijja kujenga mashirikiano na sio mashindano wakielewa kuwa huko kufuata njia ya Mwenyezi Mungu kwa kutegemea malipo kutoka kwa Mola.
Kuhusu kuwalinda vijana na dawa za kulevya Dk Shein amesema Serikali yake kupitia kamisheni ya kupambana na dawa za kulevya iliopo katika ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais imejipanga vizuri kuhakikisha kuwa vita dhidi ya Madawa yakulevya hapa nchini zinafanikiwa.
Amezipongeza Taasisi binafsi zinazoshughulia walioathirika na madawa yakulevya kwa jitahada zao za kuwakusanya vijana hao ili watokane na tatizo lautumiaji wa madawa hayo zikiwamo Zanzibar youth forum,Drug Free Zanzibar na Jumuiya Yatawabina ambapo hivi sasa Zanzibar ina jumla ya Nyumba tisa ambapo kila moja ina vijana kati ya kumi na tano hadi ishirini.
IMETOLEWANA HABARI MAELEZO PEMBA
6/11/2011
No comments:
Post a Comment