Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe |
Tangu uchaguzi wa Meya ulipofanyika Arusha na Chadema kuususia, siasa za jiji hilo zimebaki kuwa ni tete na pengine ndio maana kila inapotokea sababu basi wale wanaohisi kwamba walionewa wanapata mwanya wa kupenyezea hisia zao.
Vurugu za hivi majuzi zilizoelezewa kwamba zinatokana na kile viongozi wa Chadema walichodai kwamba ni manyanyaso ya muda mrefu kutoka kwenye vyombo vya dola ikiwamo polisi na mahakama ni kielelezo tosha cha haya ninayoyasema.
Kabla ya polisi kuwafurumusha pale kwenye viwanja vya NMC, wao walidai kwamba wangekesha pale kwa siku tatu mfululizo kushinikiza mbunge wao Godbless Lema atolewe rumande.
Hata hivyo polisi hawakukubaliana na hali hiyo na yalitokea yaliyotokea ambapo takribani watu 30 wakiwemo viongozi wa ngazi za juu wa chama hicho walikamatwa na kufunguliwa mashtaka.
Baadae, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alizungumza, akasema kwamba suala la Arusha limekosa ufumbuzi kwa kuwa Chadema hawaonyeshi utashi wa kisiasa wa kulimaliza. Wao Chadema kwa upande wao nao wakadai kwamba upande wa pili ndio hautaki kulimaliza.
Lakini kimsingi walio wengi wangekubali kwamba vurugu zile hazikuwa na umuhimu kwa kuwa Mhe Lema alipewa nafasi ya kupata dhamana lakini akakataa mwenyewe na alipo omba tena akapangiwa tarehe 14 Novemba (Kesho) kwamba afike mahakamani na wadhamini wawili.
Kwanini Chadema walilazimisha kwamba Mahakama imtoe Lema siku ile walio taka wao? Mbona mahakama haikumlazimisha Lema atoke siku ile alipokataa kutoka?
Kuna mambo ambayo wakati mwingine yanaleta utata, utata haswa kwenye malengo wanayokuwa nayo wanasiasa wakati wanapotaka kufanya mambo yao, wanaandaa mazingira ya kuungwa mkono hata kwa mambo yasiyokuwa na msingi.
Sasa cha ajabu ni kwamba baada ya kuwachochea watu, kuwapandisha munkari na viongozi kujitapa kwamba wapo tayari kufa kwa kutetea haki , mwisho wa siku viongozi hao hao wanasema kwamba suala la Arusha litamalizika kwa mazungumzo.
Kama kweli wanafahamu hivyo kwanini walifanya hayo waliyoyafanya? Kwanini baada ya kuwaingiza watu kwenye matatizo ndio kiongozi anasema kwamba ipo haja ya kufanya mazungumzo kuondoa tofauti kati ya pande mbili?
Hii ni ishara kwamba tangu mwanzo kuna kitu kilikwenda ndivyo sivyo. Lakini tutaendelea hivi mpaka lini? Nadhani imefika wakati sasa wanasiasa wawe na hoja za msingi za kusimamia la sivyo itafika wakati wananchi watachoshwa na siasa za fitna na matokea yake wapinzani wataonekana ni watu wa kuzua na waongo.
Katika nchi kama hii ambapo vyama vya upinzani vimekuwa na historia ya kupanda na kushuka kama mawimbi ya bahari, chama cha upinzani chenye nguvu kinatakiwa kufanya mambo kisayansi zaidi ili kiwe tofauti na wengine ambao wameshashuka.
1 comment:
hii kwakweli imetulia lkn ingekuwa vizuri zaidi wananchi waliowengi waisome waelewe nimejaribu kufanya uchunguzi wa kina vijana wengi hawajui historia nzuri ya viongozi wa chadema mimi bahati mbaya nipo nje yanchi ninawaelewa vizuri watu hao ukizingatia hata umri nilionao upo ni miaka 45 wengi nimewaona hao na kuona shuhuli zao walizokuwa wanazifanya kuanzia kabla yakuwa wanasiasa mpaka wanajiingiza kwenye mambo ya siasa kunawatu wanadhani mtu mkweli lazima awe mbishi wa serikali na lazima akihutubia lazima awasilishe mada yake kwa jazba na mpaka mishipa ya shingo imkakamae hatuhitaji jazba wala nguvu kwenye siasa mwanasiasa wa kweli sio mzushi wala muongo na haitaji kutafuta soko la kupendwa na watu kwani watu wenyewe humuona anafanya nn jukwaani na kwajamii inayo mzunguuka poleni sana wana wa arusha mji ni wenu wachaga wanawatawala hamjisikii vibaya?uzuri minimsukuma tena wa shinyanga sisi kawaida yetu hata sikumoja ingawa jimbo langu na mkoa wangu unawabunge wengi wa upinzani wengi kuliko mkoa wowote hapa tanzania bara huwa hatukubali kutawaliwa na mtukutoka mkoa mwingine wowote hata mkuu wa mkoa ukimleta mtu ambae hana asili yetu hapawezi na ataondoka tu na huwa hatukubali kushawishiwa na watu wa mikoa mingine ni ngumu arusha vipi?nyie si wajanja?iweje leo mtawaliwe?kuweni macho mjiwenu ni mzuri na unasifa kubwa kuliko kilimanjaro
Post a Comment