Harakati za kupinga matumizi mabaya ya madaraka na rushwa zinazoambatana na maandamano makubwa maarufu kwa jina la “Occupy Wall Street“ zimepamba moto huko Marekani ambako kutoka Wall Street, New York, tayari zimeenea kwenye miji 847. Maandamano na harakati hizo zimeanza wiki nne zilizopita bila kupumzika mpaka sasa. Hali inayoelezewa kuwa ni tete na pengine inaonekana kua ni sawa kabisa na ile ya nchi za Kiarabu za Africa maarufu kama ‘Arab Spring’.
Wataalamu wa masuala ya uchumi pia wameelezea kwamba wananchi wengi wa Marekani wamechoshwa na hali mbaya ya kiuchumi na wanaulalamikia utawala wa Rais Barack Obama kwa kushindwa kutekeleza ahadi zake kwa wananchi.
Kwa mujibu wa taarifa za vyombo mbalimbali vya habari, huko Chicago polisi wamewakamata raia 100 baada ya kugoma kutii amri wakati wa muendelezo wa maandamano hayo. ANGALIA PICHA ZIFUATAZO.... |
No comments:
Post a Comment