Millya |
Siasa za Arusha Mjini zinazidi kua tete kadri siku zinavyokwenda. Kumeshuhudiwa matukio mengi ya ghasia za kisiasa tangu ulipomalizika uchaguzi mkuu wa mwaka jana uliompa ushidi mgombea kwa tiketi ya Chadema, Bw Godless Lema.
Suala la uchaguzi wa Meya wa jiji hilo lilipelekea kumwagika kwa damu baada ya kile kilichodaiwa kua ni maandamano haramu yaliyofanywa na Chadema kuonesha hisia zao za kuupinga uchaguzi wa Meya kwa madai kwamba Chadema hawakushiriki.
Hata hivyo mwisho wa siku Chadema waligeukana wenyewe kwa wenyewe mara baada ya madiwani wake kukubaliana kuingia kataika maridhiano na CCM juu ya uongozi wa Halmashauri. Msimamao ambao ulipelekea uongozi wa juu wa Chama hicho kuwatimua madiwani wake.
Baada ya kimbunga hicho cha Chadema, juzi yameibuka mengine mapya kabisa, ambapo kundi la wafuasi wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) kutoka wilaya mbalimbali za Mkoa wa Arusha lilizingira Makao Makuu ya Polisi Mkoa ambako mwenyekiti wao, James Millya alikwenda kujisalimisha.
Licha ya shamrashamra, hamasa na kuimba wakati wakiwa nje ya makao hayo ya polisi, vijana hao walimsindikiza kwa maandamano mwenyekiti wao hadi kwenye ofisi za chama chao mara baada ya kutoka kwenye mahojiano hayo ambayo yaliripotiwa kuchukua takribani dakika 15.
Swali kubwa la kujiuliza hapa; Kwanini wafuasi hawa waliachiwa wafanye hayo waliyoyafanya bila kutawanywa na polisi?
Mambo kama haya yanajenga tabaka baiana ya wafuasi wa vyama vya siasa kwa kuwa polisi wamekuwa wakiyatawanya maandamano ambayo hayana baraka zake au mikusanyiko ambayo haina kibali cha polisi.
No comments:
Post a Comment