Leo ni siku ya furaha na faraja kwa siasa za Israeli na Palestina ambapo mpango wa kubadilishana wafungwa umeanza kutekelezwa.
Mpango huo umejumuisha kuachiwa kwa Mwanajeshi mmoja wa Israeli, Gilad Shalit na maelfu ya wafungwa wa Kipalestina waliokua wakitumikia vifungo huko Israel.
Taarifa zinasema ilikua ni nderemo na vifijo huko Ukanda wa Gaza na Kingo za Magharibi (West Bank) ambako ndugu na jamaa walikusanyika kuwapokea.
Gilad Shalit (25) ametumikia kifungo miaka mitano, jitihada za kuponya roho yake, zimeponya roho zaidi ya elfu moja za Wapalestina. |
Kwa ujumla Israeli inategemewa kuwaachia wafungwa 1,027 na kwa awamu ya kwanza itawaachia 477. Wafungwa hao wanaachiwa ikiwa baadhi yao wamekaa ndani zaidi ya miaka 30.
Wachunguzi wa hali ya mambo wamesema huenda hatua hiyo ikapunguza uhasama wa kisiasa uliopo kati ya Palestina na Israel.
No comments:
Post a Comment