Hapa Meya wa Manispaa ya Moshi, Jaffari Michael (CHADEMA) amefunga mtaa (Chagga Street), anajibu hoja za CCM walizo zitoa huko Boma Mbuzi hivi karibuni kwamba ndani ya mwaka mmoja Chadema wamepewa halmashauri na hawajafanya chochote cha maana.
Majibu ya Michael yalikua hivi "Wanatutuhumu sisi mwaka mmoja, wao wamefanya nini ndani ya miaka hamsini ya uhuru?" wananchi wakashangilia. Hii imekua kasumba, kwamba wanasiasa wanajibu shutuma kwa shutuma na kwa kua imezoeleka basi kawaida imekua kama sheria. |
No comments:
Post a Comment