Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama |
Serikali Mkoani Kilimanjaro imewaahidi wananchi wa Wilaya ya Rombo kuwa tatizo la mgogoro kati ya binadamu na wanyama pori hususani tembo ambalo limekuwapo wilayani humo kwa muda mrefu litapatiwa ufumbuzi wa kudumu ili kuhakikisa usalama wa raia wa wilaya hiyo na mali zao.
Ahadi hiyo imetolewa leo na Mkuu wa mkoa wa kilimajaro Mheshimiwa Leonidas Gama alipokuwa katika ziara ya kikazi katika kituo cha kudhibiti uharibifu wa wanyamapori kalichopo katika kijiji cha Ngoyoni katia tarafa ya Mengwe wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro.
Tayari serikali Mkoani Kilimanjaro kwa kushirikiana na Kikosi cha Kupambana na Ujangili kutoka Mkoa wa Arusha imejenga kituo cha kuzuia wanyamapori aina ya tembo katika kijiji cha Ngoyoni ambacho kitasaidia madhara ya wanyama hao kwa binadamu bila ya kuwaua au kuwadhuru wanyama hao kwa namna yoyote.
Ili kuhakikisha kuwa mradi huo ambao ujenzi wake umeshatekelezwa kwa kiasi kikubwa unakamilika mapema iwezekanavyo Mheshimiwa Gama amesema atawaita wahusika ofisini kwake ili ajue ni kwa nini kasi ya utekelezaji wa kituo hicho imekuwa ndogo.
”Sijaridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi huu kwani naona imekuwa ndogo ikilinganishwa na umuhimu wa mradi wenyewe” alisisitiza Mheshimiwa Gama.
Mheshimiwa gama alitoa ahadi hiyo mara baada ya kupokea taarifa iliyowasilishwa kwake na uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo ambayo imeeleza kuwa kuanzia mwaka 1992 hadi sasa matukio ya uharibifu mkubwa wa mazao,makazi pamoja kupoteza maisha kwa baadhi ya wananchi yamekuwa yakitokea.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo maeneo yaliyopata madhara makubwa ya wanyamapori hao ni pamoja na Holili, Mamsela Chini,,Shimbi, Ibukoni,,Msaranga,Kirongo chini na hifadhi ya misitu ya Rongai.
Mbali na hilo Mheshimiwa Gama amewapongeza wananchi wa kijiji cha ngoyoni kwa moyo wa kujitolea katika kutekeleza miradadi ya maeneleo kwa kuchangia ardhi yenye ukubwa wa eneo upatao heka moja na robo kwa ajili ya mradi wa kujenga kituo cha hicho cha kudhibiti uharibifu wa mali,makazi na mazao unaofanywa na wanyamapori hao.
Akitoa ufafanuzi wa namana mgogoro huo baina ya binadamu na wanyamapori Mkuu wa wilaya ya Rombo Mheshimiwa Peter Toima Kiroya amesema kuwa Wilaya ya Rombo ipo katikati ya hifadhi za wanyamapori hivyo basi, njia wanazopita tembo hao ambao hutokea katika hifadhi za nchi jirani ya Kenya na kuingia katika Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro (KINAPA) ni njia zao za asili zilizokuwepo tangu zamani.
Aiha Mheshimiwa Kiroya amesema kuwa takika kipindi cha miaka 30 iliyopita binadamu wameongezeka na kujikuta wanalima na kujenga katika njia za wanyama hao jambo ambalo limesababisha kuwepo kwa mgogoro huo wakati tembo hao wanapotaka kupita katika njia zao zao hizo kwa ajili ya kujitafutia chakula na maji.
(Habari kwa hisani ya Mdau Shaaban wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Kilimanjaro)
No comments:
Post a Comment