![]() |
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Balozi wa Denmark aliyemaliza muda wake wa kazi nchini Bw. Bjarne Henneberg Sorensen Ikulu jijini Dar es salaam jana. Picha na IKULU |
Wednesday, 30 November 2011
RAIS KIKWETE AMUAGA BALOZI WA DENMARK
Monday, 28 November 2011
WENGINE WAJIFUNZE KWA CHADEMA
![]() |
| Bendera ya Chadema |
Majadiliano kati ya Rais Jakaya Kikwete na Viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) yamemalizika Ikulu mchana huu baada ya kuendelea kwa siku ya pili leo.
Kimsingi Rais Kikwete anastahili pongezi kwa kukubali kuwaalika viongozi wa Chadema Ikulu, lakini kwa upande mwingine Chadema wameonyesha ukomavu wa kisiasa na nia yao ya kutaka kujenga demokrasia ya kweli nchini.
Hata hivyo picha zilizotoka kwenye vyombo vya habari mbalimbali zikionyesha tukio hilo la kihistoria, zinakuja na somo kubwa sana kwa jamii pana ya Watanzania juu ya mtizamo unaozidi kujengeka sasa ya kwamba hakuna kinachowezekana bila maandamano.
Sasa tumejifunza kwamba kumbe hata kwa njia ya amani ujumbe unafika kwa uongozi wa ngazi ya juu na kwa amani na utulivu bila kusababisha usumbufu wowote kwa watu wala kufanya uharibifu wa mali ambao mara nyingi hutokea wakati wa maandamano.
Ni wakati muafaka sasa kwa wengine wenye madukuduku yao waige njia hii ambayo Chadema wameionyesha badala ya kutangaza shari ambazo mwisho wa siku wanachi wa kawaida ndio watakao umia.
INASEMEKANA WAZO LA KUMUONA JK IKULU LILIIBULIWA HAPA!!!!!
TAARIFA YA IKULU KUHUSU MKUTANO WA CHADEMA NA RAIS KIKWETE
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wa Serikali yake leo, Jumapili, Novemba 27, 2011, amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar Es Salaam, yamefanyika katika mazingira ya urafiki na ujumbe wa CHADEMA umewasilisha mapendekezo yake kuhusu mchakato wa kuandika Katiba Mpya ya Tanzania. Serikali imepokea mapendekezo hayo.
Hata hivyo, pande zote mbili zimekubaliana kukutana tena asubuhi ya kesho, Jumatatu, Novemba 28, 2011, ili kuipa nafasi Serikali iweze kutafakari mapendekezo hayo.
Lakini pande hizo mbili zimekubaliana kuwa Katiba ya sasa ni Katiba nzuri iliyolilea Taifa kwa miaka 50 iliyopita kwa sababu ni Katiba ya sasa iliyoliwezesha Taifa la Tanzania kuwa na amani, utulivu na kupata maendeleo makubwa ambayo nchi yetu imepata mpaka sasa.
Pia pande zote mbili zimekubaliana kuhusu umuhimu wa kutunga Katibu Mpya kama Mheshimiwa Rais Kikwete alivyoliahidi taifa wakati wa salamu zake za mwaka mpya Desemba 31, mwaka jana, 2010, Katiba ambayo italiongoza Taifa la Tanzania kwa miaka mingine 50 ijayo.
Katika mazungumzo hayo, Mheshimiwa Rais aliwahakikishia wajumbe hao wa CHADEMA wakiongozwa na Mwenyekiti wa chama hicho, Mheshimiwa Freeman Mbowe kuwa ni dhamira yake na ya Serikali yake kuhakikisha kuwa Tanzania inapata Katiba mpya.
Katika mkutano huo, pande zote mbili zimekubaliana kuwa ni jambo muhimu sana kwa mchakato mzima wa kutungwa kwa Katiba Mpya kuendeshwa kwa namna ya kulinda na kudumisha tunu za taifa za amani, utulivu na umoja wa kitaifa.
Aidha, pande zote mbili zimekubaliana kuwa mchakato huo uendeshwe kwa kuzingatia misingi ya mambo mengine muhimu kwa taifa la Tanzania kama vile kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa amani, kuligawa Taifa kwa misingi ya udini na ukabila ama kutugawa kwa misingi ya maeneo.
IMETOLEWA NA:
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU
NOVEMBA 27, 2011
DAR ES SALAAM
Thursday, 24 November 2011
LA MAGAMBA; CCM BADO INAHITAJI PILIPILI KUUNGIA MBOGA
Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (NEC-CCM) inamaliza kikao chake leo huko Dodoma.
Kikao hicho cha siku mbili ambacho kilitanguliwa na vikao vya Kamati Kuu (CC) kinamalizika huku vyombo vya habari mbalimbali vikiendelea kuibua labdalabda kuhusu hatma ya chama hicho ambacho kwa sasa ndicho kinachoongoza nchi.
Kwa hakika zimekua siku kadhaa za kurushana roho, kupandishana na kushushana presha lakini yote kwa yote inaonekana mambo ni magumu kuliko watu wanavyodhani.
Wapo watu ambao wanafikiria kwamba itakua jambo rahisi kwa CCM kuwatoa kafara watu wanaotajwa kwenye kashfa mbalimbali bila kusoma alama za nyakati, lakini wapo ambao wanaona kwamba kisiasa kufanya hivyo sio suluhisho.
Na kwa maneno ya Mwenyekiti wa CCM ambaye pia ni Rais wa Nchi, Jakaya Kikwete aliyoyatoa kwenye mkutano wa NEC jana kuwataka wajumbe wawe na amani na kuwaeleza kwamba CCM ni chama kikubwa na hakuna kitakacho haribika, ni ishara tosha kwamba hilo la ‘kuvuana magamba’ kwa minajili ya ‘kuwajibishana’ halitakuwepo.
Kinachoonekana hapa ni kwamba hata kama pilipili ni kali lakini bado inahitajika kuungia mboga.
Wednesday, 23 November 2011
LA KATIBA MPYA: JK ASHAURIWA AKUTANE NA WAPINZANI WOTE
![]() |
| NAPE |
Wajummbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CC-CCM) wamemshauri Rais Jakaya Kikwete akutane na kufanya mazungumzo na vyama vyote vya upinzani badala ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) pekee.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amewaambia waandishi wa habari Dodoma jioni hii kwamba wajummbe hao wamemshauri Rais Kikwete akutane na viongozi wa vyama vyote vya upinzani haswa vile vyenye wabunge.
Nape alisema kwamba kwa ujumla wajumbe wa CC kama ilivypkuwa kwa Rais Kikwete, wamefurahishwa na hatua walio ichukua Chadema kuomba kuonana na kiongozi mkuu wan chi ili kujadiliana juu ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011.
Subscribe to:
Posts (Atom)

























