Na Iddi Haji Issa, Maelezo Zanzibar
Wito umetolewa kwa taasisi zote zisizo za kiserikali kubadilika kwa kutekeleza shughuli zilizo na manufaa kwa umma kuliko kwa mwanachama mmoja mmoja.
Wito huo umetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Asaa Rashid wakati wa ufunguzi wa mradi wa kuongeza uelewa juu ya sera ya jumuiya zisizo za kiserikali (NGOs) Zanzibar katika ukumbi wa chuo cha elimu mbadala Rahaleo
Alisema kuwa jumuiya zisizo za kiserikali zinalo jukumu kubwa katika kutekeleza wajibu wake hii inamaana kuwa iwapo Serikali itafanya kazi yake , sekta binafsi nazo zikafanya kazi yake bila shaka mafanikio yatakuwa makubwa.
Kwa upande wa Wizara katibu amesema wamedhamiria kukiimarisha kitengo cha jumuiya na hivi karibuni wanatarajia kufanya kazi muhimu za kupitia sheria ya jumuiya ( sheria Nam 6 ya 1995) ili kukiwezesha kuwafikia zaidi walengwa ambao ni jamii.
Aidha ameziomba taasisi zote kufahamu kuwa sera hiyo inatoa mwelekeo wa tunakotaka kuelekea lakini sheria imebainisha zaidi yale yaliotajwa katika sera.
Katibu huyo amesema Sheria inazitaka jumuiya zote kuelekeza kikamilifu suala zima la kuhakikisha ripoti za hesabu za jumuiya zinawasilishwa na kuangaliwa kwa usahihi wa hali ya juu.
Aidha akichangia mradi huo Mwenyekiti wa Umoja wa Wavuvi wa Kojani ( KOFDO) Omari Muhammed Ally ameiomba Serikali kutokuangalia upande wa ardhi tu ila na upande wa bahari utizamwe kwani hali inazidi kua mbaya sambamba na kuwashirikisha Wavuvi kikamilifu katika kuundwa sheria zinazo husu maswala ya bahari.
Mradi huo ambao umeanza hivi karibuni unategemewa utaendeshwa kwa muda wa mwaka mmoja chini ya Zanzibar Current Generation Forum ZCGF
No comments:
Post a Comment