Pantoni huwa kwa kiasi kikubwa ni huduma sio biashara ndio maana huko Mombasa abiria wote wanavuka bureeeee, sasa hapa walikua wanachangia 100/- serikali inasema ni ndogo sana haitoshi kujiendesha kibiashara.
Na iweje wakati wao wanapandishiana posho kwa asilimia miambili huko mjengoni msukuma mkokoteni na guta wamuongezee gharama za kuvuka Kigamboni kwa asilimia mia tano?
Kama maisha ni magumu kwa wabunge, basi ni magumu zaidi kwa wananchi wa kawaida na kwahiyo jitihada zozote za kumkaba mtanzania masikini lazima zipingwe kwa juhudi zote.
Serikali ni kama baba haipendezi baba anajua kabisa mtoto ana hali ngumu halafu anazidi kumwekea mazingira magumu ili ashindwe kabisa kuishi.
No comments:
Post a Comment