Sunday, 15 January 2012

ALIYEMPA MTEMA LESENI YA UDEREVA HAKUMTAKIA MEMA

Marehemu Mtema enzi za uhai wake.
Ni huzuni, majonzi na kwa wana familia ni pigo ambalo hawatalisahau milele. Ndio ameondoka, kwa sisi tunaoamini ‘kudra’ tunasema kwamba siku zimefika ama kwa imani ya marehemu tunaweza kusema ‘Bwana ametoa na Bwana ametwaa……”.
Naandika mistari hii ikiwa ni masaa kama 28 hivi yamepita tangu Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema) Regia Mtema afariki dunia jana pale karibu na Daraja la Ruvu barabara ya Morogoro, Mkoa wa Pwani kwa ajali ya gari.
Binafsi nimesikitika sana, nimesikitishwa na mambo mawili makubwa: 1. Mtema alikua bado kijana na alikua na matarajio mengi lakini Watanzania walikua na matarajio makubwa zaidi kutoka kwake. 2. Nimesikitishwa na taarifa kwamba marehemu alikua anaendesha gari mwenyewe.
Sote tunafahamu kwamba Mtema alikua mlemavu, hakua na mguu wa kulia ambao kwa magari ya auto ndio unaotumika kuendeshea.
Cha kushangaza ni kwamba pamoja na ulemavu huo bado Mtema alipewa leseni ya kuendesha gari na akawa anaendesha kwenye safari ndefu na kwenye barabara ambayo ina msongamano mkubwa kama hii ya Dar-Chalinze.
Nani kati yetu amewahi kujaribu kuendesha gari kwa mguu wa kushoto na akaona ugumu wake?, kwa kweli sio kitu rahisi hata kidogo.
Hata alipokua akitoa taarifa kwa waandishi wa habari jana, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani Pwani, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Salehe Mbaga alieleza wazi kwamba kilichochangia kutokea kwa ajali ile ni ulimevu wa dereva akisema kwamba haikua rahisi kutumia mguu ule kufanya maamuzi ya haraka na sahihi.
Sasa tujiulize; nani alitoa leseni kwa marehemu? Taratibu gani za kisheria zilifuatwa mpaka akaonekana anastahiki? Bila shaka tumejifunza kitu kwa tukio hili la kusikitisha.
Kwahiyo wakati tunapita katika kipindi hiki cha majonzi na huzuni, tulitafakari na hili.

4 comments:

Anonymous said...

Mimi nadhani leseni class D anaweza kupata mtu yeyote, ili mradi awe amejaribiwa na kuonekana kuwa anaweza kuendesha gari. Haijalishi atatumia mkono, kichwa, bega, wala nini. Labda tunapokuja kwa class C hapo itabidi mtu uwe fiti kwa kila idara, masikio, macho, miguu na mikono. Maana sasa hapo unapata leseni ya kuendesha vyombo vya abiria wengi, daladala, tax, na mabasi

Anonymous said...

Huu ni upuuzi. unaonyesha jinsi thinking capacity ilivyokuwa chini. disable a capable of doing wonders using their limited body parts. If you cannot consider this then i can see how low reasoning capacity one is. there are cars for disable and some minor adjustment can be made to enable them drive even motorcycles. thinki twice brother.

Anonymous said...

Kuna watu wengitu ambao ni walemavu still they can drive cars.Nawengine wanaoperate hata ndege! Kwakuwa wewe umezoea kutumiamguu wa kulia sio wote ambao wanatumia mguu huo. Hebu acha ujinga iliyobaki tumuombee marehemu.Kwani njia ya wote yeye ametangulia nasi tutafatia..

Anonymous said...

inawezekana ukawa right ukiongelea swala la long trip,ila issue ya leseni ni haki ya yule anayeweza kuendesha na kujua sheria ila limitations zipo,hasa hata leseni zina kikomo cha abiria kulingana na aina ya gari,inabidi tuangalie hilisuala kwanini ukifikia cheo/hadhi unahitaji kuwa na professional driver?na hasa kama hizi safari,nafikiri ni kutokana na majukumu mengi na mgawanyo wa kazi inabidi uwe na msaidizi,macho kwa wenzetu wenye dhamana na vyeo toeni ajira jipunguzieni mizigo kwa kazi kama hizi za kuendesha magari