Wakati mijadala ikiendelea juu ya kufukuzwa uanachama kwa Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi), mbunge huyo ameibuka na kudai kwamba yeye bado ni mbunge na kwamba mwishoni mwa wiki anatarajia kutembelea jimbo lake.
Hata hivyo Mbunge huyo amekiambia kituo cha Televisheni ya Taifa (TBC 1) kwamba hayupotayari kuzungumzia taratibu nyingine zinazoendelea ndani ya chama chake.
Wakati huohuo ripoti kutoka katika ofisi za Bunge zinasema hakuna taarifa rasmi zilizowasilishwa juu ya kuvuliwa uwanachama Kafulila.
No comments:
Post a Comment