Waziri wa Katiba na Sheria, Celina Kombani.
Vurugu zilizojitokeza Dar es Salaam na Dodoma jana zianonyesha kua tunahitaji utaratibu mzuri zaidi wa kuwafanya wananchi waweze kutoa maoni yao juu ya mchakato wa kuandikwa kwa katiba mpya.
Ni ukweli usiopingika kwamba wananchi wengi wamehamasika na kwa hivyo tunahitaji kua na sehemu kubwa zenye nafasi kama pale Jangwani (Dar es Salaam) na Jamhuri Stadium (Dodoma).
Lakini pia tunahitaji kua na mwongozo wa namna ya kutoa maoni yetu. Hii inatokana na ukweli kwamba baadhi ya viongozi wa siasa wanakwenda kwenye midahalo hii kwa kofia za vyama vyao na wanatoa maoni kwa mtazamo wa kichama zaidi bila kujali maslahi ya umma.
No comments:
Post a Comment