Ikiwa ni muda mfupi tangu waasi wa Libya wajigambe kuutwaa mji mkuu wa nchi hiyo-Tripol, tayari vitendo vya kinyama kwa watu weusi (wasio waarabu) vimeripotiwa kushika kasi.
Baathi ya wachambuzi wanajiuliza iweje mapinduzi yaliyokusudiwa kuwakomboa wanyonge (kama wanavyodai waasi) yaishie katika unyama wa kuwabaka na kuwachinja wanyonge?
|
Kiongozi wa Baraza la Mpito la Libyan (NTC) Mustafa Abdul Jalil |
Weusi hao ambao walikimbilia Libya kutafuta maisha mazuri wakati wa Gadafi na wengine wakitafuta njia ya kuendea Ulaya, waliishi kwa furaha na amani chini ya utawala wa Gadafi lakini sasa wanakiona cha moto.
Iweje Waafrika wabaguliwe Afrika na hakuna mtu wa kuwasemea?, viongozi wa Umoja wa Afrika (AU) kwanini wanalifumbia macho suala hili?
No comments:
Post a Comment