Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Baba Mtakatifu Benedict XVI ameeleza kufurahishwa na kuridhishwa kwake na amani, utulivu na uvumilivu wa kidini ulioko baina ya dini mbalimbali nchini.
Rais Jakaya Kikwete (Kulia) akimkaribisha Ikulu Balozi wa Makao Makuu ya Baba Mtakatifu ya Vatican katika Tanzania anayemaliza muda wake, Mhashamu Askofu Mkuu Joseph Chennoth. |
Kwa mujibu wa Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu msimamo huo wa Papa Benedict umetolewa Alhamisi wiki hii na Balozi wa Makao Makuu ya Baba Mtakatifu ya Vatican katika Tanzania, Mhashamu Askofu Mkuu Joseph Chennoth.
Mhashamu Askofu Mkuu Chennoth alikuwa anamuaga Rais Jakaya Kikwete baada ya kumaliza muda wake wa uwakilishi wa Vatican katika Tanzania.
Askofu Mkuu Chennoth amefanya kazi nchini miaka sita ikiwa ni sehemu ya miaka 15 ambayo ameiwakilisha Vatican katika nchi mbalimbali Afrika.
No comments:
Post a Comment