Monday, 2 May 2011
Kifo cha Osama bin Laden, Marekani imejipalia makaa.
Ni asubuhi ya Jumatatu, nimeamka najiandaa kwenda kazini baada ya likizo fupi ya wiki mbili ambayo niliitumia kidogo hapa Dar es Salaam na Kilimanjaro kijijini kwetu.
Naam kama ilivyo ada, nawasha TV nipate kujua yaliyojiri duniani kabla sijakumbana na mihangaiko na majukumu ya kiofisi.
Kwa kuwa kabla sijalala nilikua natizama BBC World, Tv inawaka na channel ya kwanza kuiona ni BBC, Macho yanakutana na maneno makubwa kabisa Breaking News, napatwa na shauku ya kufahamu zaidi, nafikicha macho ili nione vizuri: Naama inasomeka hivi 'US Media: Osama bin Laden Found dead by US forces".
Ni habari kubwa, kubwa sana kwa kweli na inastahiki kua Breaking News kama ilivyo, mtangazaji anasema ni habari zinazosubiria kudhibitishwa na Rais wa Marekani, Barack Obama.
Bado nasubiri kua miongoni mwa watu wa mwanzo kabisa kupashwa habari, siendi kuoga mpaka nijue kinaga ubaga, punde si punde TV inaonesha chumba ndani ya Jumba Jeupe (white house) kuna nembo ya Ikulu kwenye sakafu na bendera mbili na mike mbili zinasubiri mkuu aje kupazia sauti.
"Osama amekufa" ni kauli ya kwanza kabisa niliyoisikia kutoka kwa Obama, ni kauli nzito, kauli iliyobadili fikra za wengi kwamba Osama asingekamatika, ni kauli aliyoisema kwa kujiamini sana kiasi cha wananchi wa Marekani kujaa nje ya Ikulu kwa mamia wakishangilia kile walichokiita ni ushindi baada ya miaka takriban kumi ya kumsaka Osama.
Suala la msingi hapa na muhimu kujiuliza kila mmoja wetu ni kwamba, hivi ni kweli Marekani kwa kumuua Osama inajiwekea mazingira yakuwa salama zaidi?
Wachunguzi wengi wa hali ya mambo tayari wameonyesha wasiwasi wao, wanasema Marekani na washirika wake wamejiweka papaya zaidi kwa kifo cha Osama kwa kuwa mtandao sio mtu, Osama alikua kiongozi tu, yani kama rimoti ambayo kuwepo au kutokuwepo kwake hakuzuii TV kufanya kazi.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, tayari wafuasi wa Osama wamesema kwamba ikiwa habari za kifo cha mkuu wao ni za kweli basi marekani na wamarekani wasubiri cha mtema kuni.
"Oh God, please make this news not true... God curse you Obama," said one message on an Arabic language forum. "Oh Americans... it is still legal for us to cut your necks."
"Osama may be killed but his message of Jihad will never die. Brothers and sisters, wait and see, his death will be a blessing in disguise," said a poster on another Islamist forum.
Maneno kama haya yanaashiria kwamba kama ni kidonda basi Marekani wamekitia chumvi na sasa kinavia damu. Huu huenda ukawa mwanzo wa ugaidi mwingine mkubwa sana duniani na kimsingi tutaumia wote wliokuwemo na wasiokuwemo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment